
Msako waanzishwa kubaini wakuu, wamiliki wa shule wanaohatarisha afya za wanafunzi
Bukoba. Serikali mkoani Kagera imeanza operesheni maalumu ya kukagua na kuchunguza shule za msingi na sekondari za Serikali na binafsi ili kubaini walimu wakuu na wamiliki wa shule wanaokiuka kanuni za afya na usalama wa wanafunzi. Operesheni hiyo inalenga kubaini shule zenye dosari katika miundombinu ya maji safi na salama, chakula, usafi wa mabweni, na…