Wataalamu wakutana Mbeya kujadili chakula, maji na nishati

Mbeya. Wataalamu kutoka mataifa tisa wamekutana jijini Mbeya katika kongamano la kujadili changamoto zinazozikabili sekta za maji, chakula na nishati na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kongamano hilo la siku tatu, limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), linashirikisha nchi za Israel, Marekani, Kenya, Uganda, Morocco, Zambia, Ethiopia, Malawi na Tanzania ambao…

Read More

Walimu wadaiwa kuiba maharage, mahindi ya shule Makambako

Njombe. Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Magegele Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wameitaka halmashauri kuwachukulia hatua za kisheria walimu ambao wamebainika kujihusisha na wizi wa mahindi na maharage ya shule. Wamesema vinginevyo hawatakuwa tayari kutoa tena mchango wa chakula shuleni hapo. Kauli hiyo wameitoa leo Julai 14, 2025…

Read More

Takukuru yachunguza vyama vya siasa Mbeya

Mbeya. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Mbeya imesema inaendelea na uchunguzi kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Pia imesisitiza kuwa taasisi hiyo haichunguzi tu upande wa CCM pekee, badala yake vyama vyote vya siasa inaendelea kuvichunguza kutokana na kuwapo kwa malalamiko ikiwamo watiania…

Read More

Kibu atemwa, Taifa Stars ikijiandaa na CHAN

Kambi ya Taifa Stars inayoendelea Ismailia, Misri, imepamba moto huku maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 yakiendelea kwa kasi. Hata hivyo, kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Dennis, ameachwa rasmi kwenye kikosi. Kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ pamoja na benchi lake la ufundi…

Read More

Mchezo mchafu watiania CCM wafichuliwa

Dar/mikoani. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeanza vikao vya mchujo wa majina ya wagombea ngazi ya kitaifa, huku kikisema kimebaini michezo michafu inayofanywa na watiania, ikiwamo kuziingilia kamati za siasa na kuchafuana. Pia, kimeeleza utaratibu wake wa kupendekeza watiania, unahusisha alama A hadi E na anayepewa ya kwanza ndiye anayestahili zaidi na ya mwisho hastahili kupendekezwa,…

Read More

Bwege apata janga jingine, asisitiza haki uchaguzi mkuu

Lindi. Imekuwa bahati mbaya kwa mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini, mkoani hapa, Seleman Bungara maarufu ‘bwege’ kutokana kuvunjika mguu ikiwa ni wa pili baada ya awali kukatwa kwa sababu ya maradhi. Bwege aliyekuwa akisifika kuwasilisha hoja zake bungeni kwa njia vichekesho na utani amevunjika mguu jana Jumapili usiku nyumbani Kilwa Kivinje wakati akijiandaa kuingia…

Read More

Mitazamo tofauti uamuzi wa Polepole kujiuzulu

Dar es Salaam. Wadau wa siasa na diplomasia wamepokea kwa mtazamo tofauti uamuzi wa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole wa kujiuzulu katika nafasi hiyo huku wakiuhusisha na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Baadhi ya wadau hao wameeleza kwamba ni haki yake kujiuzulu kulingana na sababu alizonazo, hata hivyo wamebainisha kwamba njia aliyoitumia kuweka…

Read More