
Tumechanganywa na tumechanganyikana | Mwananchi
Fyatu mwenzenu niliipata kinoma. Katika kupata ulabu si akatokea chawa mmoja akamshambulia rafiki yangu ambaye ni mchunaji, sorry mchungaji wa kujipachika. Ni wakati alipokuwa akisifia ufyatu wangu ninaotoa hapa. Fyatu sorry chawa alihamaki na kurusha matusi tena ya kitoto utadhani hakuwa fyatu mzima! Nilipohoji kunani, alisema tena kwa kebehi ‘inakuwaje huyu unamruhusu achanganye dini na…