
GASSHUKU 2025 LA JUNDOKAN TANZANIA LAFANA JIJINI DAR
Wanafunzi na wakufunzi wa Jundokan Karate Do Tanzania leo Jumapili, Julai 6, 2025, wameungana katika Gasshuku – yaani semina maalum ya karate – iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Azania, jijini Dar es Salaam. Neno “Gasshuku,” lenye asili ya Kijapani, linamaanisha “kambi ya pamoja ya mafunzo,” ambapo wakarateka wa viwango…