Ecua atikisa dili la Sowah Yanga

SIKU moja baada ya Mwanaspoti kuripoti kuwa huenda straika Celestin Ecua akatua na kocha mpya wa timu hiyo anayekuja kuchukua mikoba ya Miloud Hamdi, mambo yanadaiwa kuonekana kwenda vizuri huku ikidaiwa amepindua dili la Jonathan Sowah, raia wa Ghana. Straika huyo ambaye ndiye MVP wa Ligi Kuu Ivory Coast, amemaliza msimu wa 2024-2025 akitupia mabao…

Read More

2025 haukuwa mwaka wa Simba

LICHA ya kuonyesha kiwango bora Simba imemaliza msimu ikiwa mikono mitupu, bila kutwaa taji lolote katika mashindano yote iliyoshiriki jambo linalozua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo. Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga, waliotwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Hili…

Read More

Msauzi ashikilia hatma ya Aziz KI Wydad

BAADA ya kucheza dakika 11 kwenye mechi mbili za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Manchester City na Juventus, kiungo mshambuliaji wa Wydad, Stephane Aziz KI huenda asiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao huku ikielezwa ili abaki kuna ishu anaisikilizia. Wydad ilicheza mechi tatu za michuano hiyo na kuondolewa hatua ya makundi bila…

Read More

Askofu Kinyaiya atia neno kupumzika Dk Mpango

Dodoma. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma, Beatus Kinyaiya amesema alichofanya Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kuamua kupumzika si cha kawaida kwa kuwa wengine wanang’ang’ania nafasi za uongozi. Januari 18, 2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kukubali ombi la Dk Mpango kupumzika. Katika mkutano huo,…

Read More

Samia: Tunataka amani na utulivu

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema sifa njema kuhusu utulivu na amani iliyopo Tanzania iendelezwe katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Amesema hayo leo, Julai 5, 2025, alipozindua hema (jengo la ibada) la Kanisa la Arise and Shine Tanzania linaloongozwa na Mtume Boniface Mwamposa, Kawe jijini Dar es Salaam, akigusia sifa hiyo…

Read More

Kauli Bunge sio chombo cha machawa yazua majibizano

Bariadi. Mnyukano wa hoja umeibuka, baada ya kauli ya Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliyetaka bunge lisidogoshwe kwa kuonekana ni chombo ambacho hata machawa na wachekeshaji wanapaswa kwenda kukitumikia. Kauli hiyo imemuibua Mchekeshaji, Clayton Chipando maarufu Babalevo aliyesema Zitto ametoa kauli hiyo kwa sababu amemwona amechukua fomu ya kuwania ubunge Kigoma Mjini kwa…

Read More

Profesa Mkumbo: Tiseza italeta ufanisi zaidi

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuanzishwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (Tiseza) kunalenga kuwaondolea wawekezaji usumbufu. Amesema sasa wawekezaji watakuwa na uwezo wa kupata huduma katika eneo moja tofauti na zamani walipokuwa wakienda ofisi mbili. Profesa Kitila amesema hayo leo Jumamosi…

Read More

Samia kuhutubia maadhimisho ya uhuru Comoro

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Comoro kwa mwaliko wa Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro, Azali Assoumani. Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 5, 2025 na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Shaaban Kissu imesema Rais Samia atasafiri kesho Jumapili Julai 6, 2025….

Read More

UCHAMBUZI WA MJEMA: Enock umekufa kifo cha kikatili, damu yako itumike kuimarisha utawala wa sheria

Mauaji ya kikatili ya kijana Enock Thomas Mhangwa wa mkoani Geita, yanaumiza, yanahuzunisha, yanaudhi na yanatia hasira, lakini ukweli tumefika hapo kama Taifa kwa sababu ya baadhi yetu kutojali wala kuheshimu misingi ya utawala wa sheria. Yaani tumefikia mahali watu wanaua kijana mdogo kama Enock asiye na hatia na wanapata ujasiri hadi wa kujirekodi hatua…

Read More