
WANANCHI WARIDHISHWA NA HUDUMA ZA WIZARA YA ARDHI SABASABA
Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) wameonesha kuridhishwa na huduma zinazotolewa na wizara hiyo. Wakizungumza katika banda la Wizara ya Ardhi tarehe 4 Julai 2025 katika maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Mwl Nyerere Dar es Salaam, wananchi hao…