
Waliofariki kwa ajali iliyotokea Same, wazikwa
Moshi. Mamia ya wananchi wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wamejitokeza kushiriki maziko ya watu watatu wa familia tatu tofauti waliofariki dunia katika ajali ya magari mawili ya abiria yaliyogongana na kuwaka moto wilayani humo. Miili hiyo ya Irene Salehe, Erine Ndarai na Anjela Mshana imeagwa leo Ijumaa Julai 4, 2025 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri…