Utegemezi wa Akili Unde sasa janga kwa vijana
Dar es Salaam. Katika dunia ya sasa ambapo matumizi ya akili unde (AI) yameshika kasi, jamii imetahadharishwa kuwa kuna hatari ya kizazi kijacho kikawa na maarifa mengi, lakini kikakosa uwezo wa kuishi pamoja, kuelewana na kushirikiana kijamii. Angalizo hilo limekuja ikiwa ni matokeo ya kushuka kwa kiwango cha maingiliano ya ana kwa ana miongoni mwa vijana…