Mmoja afariki, 11 wajeruhiwa wakitoka kwenye sherehe Kilimanjaro
Moshi. Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mtawa wa Kanisa Katoliki, amefariki dunia huku wengine 11 wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuligonga gari jingine kwa nyuma wakati wakitoka kwenye sherehe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo amesema ilitokea jana Julai 25, 2025 saa 1:20 usiku katika eneo…