
Nafasi za kozi za vyuo vikuu kufikia malengo ya Dira 2050
Takriban wanafunzi 125,000 ambao ni zaidi ya asilimia 99 ya waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka huu wamefaulu. Hivi sasa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu tayari zimefungua madirisha ya udahili na zinaendelea kupokea maombi ya wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo unaotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu. Hata hivyo, changamoto moja bado haijapata mwarobaini…