
Mudathir amaliza utata, atakuwepo Jangwani hadi 2027
Hatimaye kiungo Mzanzibar, Mudathir Yahya Abbas amemaliza utata wa wapi atacheza msimu ujao wa 2025-2026. Kwa taarifa rasmi ni kwamba, Mudathir ataendelea kuwa kwenye kikosi cha Wananchi hadi mwaka 2027. Hiyo ni baada ya kiungo huyo kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kusali katika kikosi hicho cha Yanga baada ya ule kumalizika mwisho wa msimu…