
Mtoto anayedaiwa kujinyonga Arusha azikwa, wazazi wasimulia…
Arusha. Mwili wa mtoto Karim Rahim (8), mkazi wa mtaa wa ‘Osunyai Jr’, Kata ya Sombetini jijini Arusha anayedaiwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya pazia, umezikwa jioni ya leo Jumatatu, Julai 21, 2025. Mtoto Karim amefariki dunia jana Jumapili, akidaiwa kujinyonga na kamba iliyokuwa imefungwa dirishani katika moja ya chumba cha kulala. Kwa mujibu wa…