
ONGEA NA ANTI BETTI: Hapa kuna ndoa au ananihadaa?
Nina uhusiano na mwanamke kwa miaka mitatu na tulipanga mwishoni mwa mwaka huu nikatoe barua kwao na taratibu nyingine ili mapema mwakani tufunge ndoa. Ila nimepata taarifa ana mume na hajawahi kuniambia, si taarifa tu bali hadi picha wakiwa wanafunga ndoa kanisani nimeonyeshwa, ninashindwa kumuuliza atasema ninasikiliza maneno ya watu na ninampenda nahofia kumkosa iwapo…