
Siku ya kulia, kucheka CCM
Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingia katika hatua ya mchujo wa mwisho wa majina ya watia nia ya kugombea ubunge, uwakilishi na udiwani, ambapo leo Jumamosi Julai 19, 2025, ndoto za baadhi ya wagombea zitafikia tamati huku wengine wakipiga hatua kuelekea kwenye kinyang’anyiro kikuu. Ni siku ya maamuzi, ambapo Kamati Kuu, inatarajiwa kuweka…