Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amepongeza jitihada kubwa na mafanikio makubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika kukuza uchumi na kuboresha miundombinu nchini.
Akizungumza Alhamisi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya kimkakati ya usafirishaji wa mizigo kwa treni ya kisasa (SGR), Bandari Kavu ya Kwala, na uwekaji wa jiwe la msingi la Kongani ya Kwala, Dkt. Kikwete alisema:
🎙️ “Hii ni ishara ya dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kuimarisha uchumi wa taifa, kuboresha miundombinu na kuleta ajira kwa Watanzania, hasa vijana.”
🔹 Dkt. Kikwete aliongeza kuwa tayari kuna matokeo chanya yanayoonekana mkoani Pwani, ikiwemo:
Kuongezeka kwa thamani ya ardhi,
Ujenzi wa miundombinu ya kisasa,
Mvuto kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
📍 Kongani ya Kwala na Bandari Kavu ya Kwala ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayolenga kuondoa msongamano wa mizigo bandarini, kurahisisha usafirishaji na kuchochea ukuaji wa viwanda.