KOCHA wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ametaja kikosi cha nyota 11 watakaoanza katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya CHAN 2024 dhidi ya Burkina Faso.
Katika kikosi hicho, Clement Mzize atakuwa anaongoza mashambulizi, akishirikiana na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Iddi Seleman ‘Nado’ watakaotokea pembeni huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akiunganisha safu ya kiungo cha ushambuliaji.
Kikosi kamili cha Stars kinachoanza ni kipa Yakoub Suleiman, huku mabeki wakiwa Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Ibarahim Abdullah ‘Bacca’ na Dickson Job.
Viungo ni Yusuph Kagoma na Mudathir Yahya wakati mawinga wakiwa Iddi Seleman ‘Nado’ na Abdul Suleiman ‘Sopu’, huku Clement Mzize akiwa mshambuliaji wa mwisho akisaidiana na Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Tanzania ipo Kundi B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati.