NAIBU KATIBU MKUU KISAKA ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU MAONESHO YA NANE NANE

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Kisaka Meena ametembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu leo Agosti 2, 2025 katika maonesho ya Wakulima ya Nanenane.

Akizungumza wakati wa kutembelea banda hilo, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake kwa elimu inayoendelea kutoa kwa umma na wadau katika maonesho hayo.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “CHAGUA VIONGOZI BORA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI 2025”