SERA ZA AIDANI KWEZI GUMZO SEGEREA, WAPAMBE WAANZA UPOTOSHAJI

:::::

Kinyang’anyiro cha kupata mgombea ndani ya Chama cha Mapinduzi kimezidi kupamba moto, wakati wagombea wakiendelea kujinadi na kuomba kura kwa wajumbe ndugu AIDANI KWEZI amendelea kufanya vizuri kupitia Sera zake zikionekana kugusa mahitaji ya Wanasegerea.

Hali hii imepelekea wapambe wa wagombea wengine kuanza propoganda za upotoshaji wakiona mwitikio na imani ya wajumbe juu ya mgombea huyu kijana.

Aidani Kwezi anaendelea kunadi sera zake huku akisisitiza wajumbe siku ya Uchaguzi kumpa kura za kishindo ili kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi Jimbo la Segerea kwa kupata muwakilishi wa kweli kwa wananchi wa Segerea.

Inaonekana Wananchi wengi wa Segerea wanahitaji mabadiliko ambapo kupitia sera za Kwezi wajumbe wengi wanaonekana kuguswa nazo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Segerea.