NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania (Taifa Stars) imeanza vizuri michuano ya CHAN 2025 baada ya kufanikiwa kuichapa Burkina Faso mabao 2-0 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo.
Katika mchezo huo ambao ulitanguliwa na shamrashamra za sherehe za ufunguzi, Taifa Stars akiwa nyumbani uwanja wa Benjamini Mkapa ameweza kucheza karata zake vizuri kwa kufanikiwa kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo muhimu.
Taifa Stars ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Abduli Sopu kwa mkwaju wa penati baada ya Clement Mzize kuchezewa rafu ndani ya boksi la mpinzani.
Bao la pili limefungwa na beki Mohammed Hussein katika kipindi cha pili cha mchezo.
Tanzania ni mwenyeji kwenye michuano hiyo ikijumuisha nchi tatu zikiwemo Kenya na Uganda ambapo leo ilikuwa ufunguzi kwa mchezo mmoja.
Kwa matokeo hayo Tanzania anaongoza kundi lake (kundi B) ambalo linatimu kama Mauritania, Madagascar, Afrika ya Kati na Burkana Faso.