BALOZI LIBERATA MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO MKUU MAALUM WA UWT, DODOMA

::::::

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa UWT Taifa, Balozi Liberata Mulamula, ameshiriki Mkutano Mkuu wa Umoja huo, ulikuwa na lengo la kuwapigia kura na kuwachagua wabunge wa Viti Maalum vya Makundi maalumu waliopitishwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkutano huo wa UWT, umefanyika jijini Dodoma ukiongizwa naa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda na viongozi wengine wa Umoja huo.