…………….
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) inashiriki Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kutoa elimu kuhusu ununuzi wa Umma kwa wazabuni, hususan elimu kuhusu Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, . James Sando, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Nelson Kessy amesema PPAA imejipanga kutoa elimu kwa wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla ili kutoa wigo mpana zaidi kwa wazabuni na wadau wa sekta hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Kessy amewasihi wadau wa ununuzi na wananchi kwa ujumla kutembelea Banda la PPAA linalopatikana ndani ya Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Maonesho haya kwa mwaka 2025 yamebeba kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”. Maonesho ya NaneNane Kitaifa yalifunguliwa rasmi tarehe 1 Agosti, 2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mapango. Maonesho hayo yalianza tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025.