Dar es Salaam. Mahakama Kuu imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana), majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kuwafanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu yao.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP), imezuia pia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.
Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini alikamatwa Aprili 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10, 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake ya kijamii.