Majaliwa atembelea banda la Yas Nanenane

Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea banda la kampuni ya Yas katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini hapa.

Akiwa katika banda hilo leo Agosti 4, 2025, Majaliwa alipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mixx by Yas Kanda ya Kati, Charles Gasper kuhusu namna kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima kupitia huduma za mawasiliano na miamala ya kifedha.

Gasper amesema ujio wa Waziri Mkuu ni ishara ya kutambuliwa kwa mchango wa Yas na Mixx katika maendeleo ya wakulima na Watanzania kwa ujumla.

“Tunayo furaha kubwa kutembelewa na viongozi, wageni na wadau mbalimbali, akiwemo Waziri Mkuu. Yas tupo na wakulima kwenye safari yao ya mafanikio,” amesema.

Yas na Mixx zimejipambanua kama wadau muhimu wa maendeleo vijijini kwa kutoa suluhisho rahisi, salama na jumuishi katika mawasiliano na huduma za kifedha, hatua inayolenga kuongeza tija ya kilimo na kuinua kipato cha wananchi.