MCHENGERWA APIGA KURA YA MAONI RUFIJI



Mohamed Mchengerwa leo Agosti 4, 2025 akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Azimio kata ya Umwe Rufiji pamoja na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa kata ya Umwe wakisikiliza maelekezo kutoka Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Wajumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya, kuelekea kupiga kura za maoni katika nafasi ya Udiwani na Ubunge Jimbo la Rufiji, Mkoani Pwani.
Wajumbe wa mkutano Mkuu wa kata ya Umwe wakipiga kura kwa amani  kumchagua Mbunge wa jimbo la Rufiji na Diwani wa Umwe.