Waliokuwa wabunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kisha kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya na Esther Mathiko, wameshindwa kuongoza katika kura maoni baada ya Wabunge wanaotetea nafasi zao Michael Kembaki wa Jimbo la Tarime Mjini na Robert Maboto wa Jimbo la Bunda Mjini, majimbo yote ya mkoani Mara, kuongoza kwa kura.
Esther Mathiko na Ester Bulaya walitia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia CCM, na kisha majina yao kuwa miongoni mwa waliopendekezwa kupigiwa kura za maoni.
Mathiko ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 196 huku Michael Kembaki anayetetea nafasi yake akipata kura 1,568.
Bulaya amepata kura 625 huku Robert Maboto anayetetea kiti chake akipata kura 2,545.