Lugangira Amkabidhi Kiti Mwendo Mama Mwenye Ulemavu Bukoba

Na Diana Byera – Bukoba

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia (CCM) Neema Lugangira, amemkabidhi kiti mwendo kipya Mama Justina, mkazi wa Mafumbo Kata ya Kashai Bukoba Mjini.

Tukio hili limefanyika nyumbani kwa Mama Justina kama ishara ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kumwezesha Lugangira kumaliza kipindi chake cha uongozi kwa amani, mafanikio makubwa, na matokeo yanayopimika.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Lugangira alisisitiza kuwa huduma kwa jamii haipaswi kutegemea nafasi ya uongozi, bali ni wito wa moyo wa kujitolea. Alieleza kuwa alianza kusaidia jamii hata kabla ya kuwa Mbunge na ataendelea kufanya hivyo kwa kuwa hiyo ndiyo imani yake ya kweli kuhusu maendeleo.

“Nitaendelea kufanya kazi na jamii kadri Mungu atakavyonifungulia njia. Huu ni wito kutoka moyoni mwangu, haijalishi kama nitakuwa Mbunge au la. Najisikia vizuri ninapotoa msaada” 

Nimefanya hivi kama sehemu ya shukrani kwa utumishi wangu wa miaka mitano wa kuwatumikia wananchi kupitia upande wa NGOs Kuchangia huduma za kijamii ndicho kitu kinachonipa furaha kubwa,”

Wananchi waliohudhuria tukio hilo walimpongeza kwa moyo wake wa huruma na kujitoa kwa jamii, wakisema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wa sasa na wa baadaye.