Mtia nia wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Ruangwa mkoan Lindi, Kaspar Mmuya apata ushindi wa kura 5986 kati ya kura 9547 na kuongoza katika kata 19 kati ya 22 zilizopo katika jimbo hilo.
Akisoma matokeo katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ruangwa Abbas Beda Mkweta,amesema kura zilizopigwa na wajumbe ni 9,547, kura zilizoharibika ni 176 na kura halali ni 9,372 ambapo amemtangaza Kaspar Kaspar Mmuya kuwa mshidi kwa kupata kura 5,986 huku wagombea wengine Fikiri Boniface Liganga akipata kura 1,591, Bakari Kalembo Nampenya kura 1,035 na Philip Undile Makota kura 660.
Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ndilo linaloongozwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Mbunge anaemaliza muda wake.
Aidha Kaspar Mmuya amewahi kuwa katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani, Naibu Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge na Uratibu, pia amewahi kuwa katibu tawala mkoa wa Dodoma.