Klabu ya Simba imethibitisha kuinasa saini ya mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Namungo Fc ikiwa ni muendelezo wa kuboresha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Mligo (17) raia wa Tanzania anatua klabuni hapo huku Mnyama akiwa na matumaini makubwa kutokana na ubora alionao na anatarajiwa kuziba pengo lililoachwa na aliyekuwa nahodha Mohammed Hussein Zimbwe Jr ambaye ameondoka klabuni hapo.