MTANDAO wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net) Wilaya ya Ilala umemtunuku tuzo maalumu Mkuu wa wilaya hiyo Edward Mopogolo ya kutambua mchango wake katika kujenga jamii salama,jumuishi na yenye usawa wa kijinsia
DC Mpogolo amekabidhiwa tuzo hiyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo.
Aliushukuru mtandao TPF Net kwa kutambua mchango huo na kwamba tuzo hiyo ni heshima kubwa kwake na wananchi wa Wilaya ya Ilala.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na SSP Latifah Chicco (RFBO Ilala),ASP Sophia Dilunga (OCS Kati na A/Inspekta Husna wa Ofisi ya RFBO Ilala.