Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera ameipongeza DUWASA na kuitaka kuendelea kutoa huduma Bora na yenye ufanisi kwa wananchi.
Dkt. Serera ametoa rai hiyo Leo Agosti 06, 2025 alipotembelea Banda la Wizara ya Maji, ambapo amepokea maelezo kuhusu huduma za DUWASA.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inashiriki Maonesho ya Nanenane Nzuguni – Dodoma.