Utambulisho wa Tshabalala Yanga wamfunika hadi Sowah

UTAMBULISHO wa aliyekuwa nahodha wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ndio wenye mapokezi makubwa zaidi dirisha hili la usajili kwa klabu za Simba na Yanga ukimpiku Jonathan Sowah wa Simba.

Tshabalala ametambulishwa usiku wa kuamkia leo Jumatano hadi sasa baada ya kupostiwa mtandao wa kijamii Instagram wadau wa soka 132k wamependezwa na utambulisho wake wakati mshambuliaji wa Simba, Sowah utambulisho wake ulikuwa na wadau 70.6k.

Sowah alitambulishwa na Simba Ijumaa baada ya kunaswa akitokea Singida Black Stars ambayo ameitumikia kwa miezi sita baada ya kuingia dirisha dogo la usajili.

Ukiondoa ushindani wa sajili hizo mbili ambazo zimeibua hisia za mashabiki wa soka kutokana na utambulisho wao nahodha huyo wa zamani wa Simba namba zake zimekuwa kubwa zaidi ya nyota wengine wote waliotambulishwa Yanga.

Wachezaji wengine wa Yanga waliotambulishwa ni Moussa Balla Conte ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa utambulisho wake ulipendwa na watu 90.5, Offen Chikola 73.2, Abdulnassir Mohamed 56.3, Pacome Zouzoua ambaye ameongeza mkataba 107k.

Wengine ni Denis Nkane 41.6k, Lassine Kouma 88.7k, Abubakar Nizar Othuman 57.5k, Duke Abuya 47.7k, Maxi Nzengeli 54.1k, Israel Mwenda 84.7k, Azizi Andambwile 41.5k, Andy Boyeli 72.8k, Ecua Celestin 59.2k, Mohamed Doumbia 53.9k.

Wakati kwa upande wa Simba nyota wengine wapya waliotambulishwa ni Rushine De Reuck ambaye aliibua hisia zaidi kwa mashabiki kutokana na kupendwa na wadau 143k ndiye mchezaji wa kwanza kutambulishwa Julai 29, 2025.

Allasane Kante alipendwa na watu 132k sawa na Tshabalala ambaye bado ajamaliza siku tangu atambulishwe huku kiungo huyo akiwa na wiki moja tangu atambulishwe, Morice Abraham 104k, Hussein Semfuko 97.6k, Mohamed Bajaber 116k na Antony Mligo 76.4k.