Mkufunzi wa Usalama na Ulinzi, Kadama Malunde akitoa mafunzo kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)
Na Eunice Kanumba – Shinyanga
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) wamepatiwa mafunzo juu ya usalama na ulinzi wa kimwili, kidijitali na afya ya akili, hususan katika kipindi hiki ambapo mazingira ya kazi ya uandishi wa habari yameendelea kuwa hatarishi.
Mafunzo hayo yameendeshwa Agosti 6, 2025 na Mkufunzi wa Usalama na Ulinzi, Kadama Malunde, ambaye ni mwandishi wa habari baada ya kujengewa uwezo na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kisha kutakiwa kuwajengea uwezo waandishi wenzao ili wawe salama katika maeneo yao ya kazi.
Malunde amesema waandishi wa habari wanapaswa kuchukua tahadhari na kujilinda wakati wote kwani ulinzi na usalama huanzia kwa mwandishi mwenyewe.
Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama wa vifaa vya kazi na kuepuka kubofya viunganishi visivyo salama mtandaoni.
“Ni muhimu kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya mashambulizi ya kimtandao kwa kuhakikisha viunganishi vinavyopokelewa vinathibitishwa kabla ya kubofya, kutumia nywila imara na kuweka uthibitishaji wa hatua mbili (Two-Factor Authentication). Ni muhimu waandishi kuwa makini zaidi, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kipindi ambacho kihistoria huongeza hatari ya vitisho, ukatili na hata kukamatwa kiholela,” amesema Malunde.
Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Stela Ibengwe wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) , Moshi Ndugulile wa Radio Faraja Fm Stereo na Suleiman Abeid wa Gazeti la Majira, wamesema yamewajengea uwezo mkubwa na sasa wanajua mbinu za kufanya kazi kwa usalama.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Empowering Journalists for Informed Community” (Kuwawezesha Waandishi wa Habari ili Jamii Iweze Kupata Taarifa Sahihi) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS), Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica.