………………….
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, Asia Juma Messos ametoa wito kwa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia vyema Taasisi zake ili ziendelee kutekeleza miradi ya Sekta ya Nishati kwa ufanisi na hivyo kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Messos amesema hayo Agosti 6, 2025 wakati alipoitembelea Banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ( Nanenane) Jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi ikiwemo miradi ya umeme na Gesi Asilia hivyo Wizara iendelee kuzisimamia Taasisi zake, ziweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkalama pia ametembelea Mabanda ya Taasisi za Wizara ambazo ni TANESCO, REA, EWURA, PURA, TPDC, PBPA na TGDC ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Maonesho hayo.
Katika ziaza hiyo Messos ameambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Mpwapwa, Michael Maganga, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala kutoka Wizara ya Kilimo, Eliasifu Mlay.