BOT YATOA ELIMU YA UDHAMINI WA MIKOPO NANENANE


 :::::::;

Na Ester Maile Dodoma 

Banki kuu ya Tanzania (BOT)  yaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusiana na mfuko wa udhamini wa mikopo ambapo mifuko hiyo imeanzishwa na serikali huku ikisimamiwa na banki kuu ya Tanzanio( BOT).

Hayo yamebainishwa na CPA Michael Mwituka ambaye ni mkaguzi wa mahesabu kwa upande wa bank kuu katika maswala ya mikopo .

Hata hivyo lengo kuu la kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa wakulima pamoja na sekta zote za uchumi ndani ya nchi .

ambapo mifuko hiyo imegawanyika katika sehemu mbili ,mfuko wa udhamini wa mikopo mauzo nje ya nchi ,wajasiliamali wadogo na wakati.

Aidha mfuko unatoa asilimia 75 ya kiasi cha mkopo kwa mikopo ya mda mfupi na asilimia 50 kiasi cha mkopo kwa mikopo ya mda mrefu.