CP. WAKULYAMBA AFUNGA MAFUNZO YA KIKOSI KAZI TAIFA DHIDI YA UJANGILI

………………..

Na Sixmund Begashe – Mtwaumbu Arusha

Maafisa wa Kikosi kazi Taifa Dhidi Ujangili (NTAP) wametakiwa kutekeleza mafunzo waliyoyapata kwa vitendo ili kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya nyara kwa ufanisi.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo washiriki kutoka Kikosi kazi hicho, kulichofanyika Mtowaumbu Mkoani Arusha.

CP. Wakulyamba ameleza kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imeamua kuendesha mafunzo hayo kwa lengo la kuboresha na kuimarisha is utendaji kazi kwa wataalam hao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia yanayotumiwa na wahalifu katika ujangili na biashara haramu ya nyara.

“Mada zote mlizofundishwa katika mafunzo ya siku tatu, ni muhimu na zitasaidia katika kupanua wigo wa kufanya kazi za intelijensia, ukamataji, upelelezi na uendeshaji mashtaka kwenye mahakama zetu kwa weledi” Aliongeza CP. Wakulyamba .

Kabla ya kufunga mafunzo hayo, CP. Wakulyamba alitoa mada inayohusu “ UCHUNGUZI WA ENEO LA TUKIO LA UHALIFU (CRIME SCENE INVESTIGATION)”. Katika Mada hiyo CP. Wakulyamba alifafanua masuala ya Kukagua, Kukusana na Kutunza Vielelezo na Ushahidi unauohusishwa na Uhalifu kwenye eneo uhalifu ulipotendeka

Aidha, Katibu wa Kikosi Kazi Taifa Dhidi Ujangili (NTAP) ACP. Jumanne Malangahe, ameushuruku Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo, na kuahidi kuwa, watayatumia vyema katika ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na misitu nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.