Idadi hiyo ya mabasi ni sehemu ya yale 250 yatakayotoa huduma katika njia hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo uliokamilika takribani miaka miwili iliyopita.
Mabasi hayo yamewasili kutoka nchini China yalikotengenezwa. Taarifa ambazo Mwananchi limedokezwa ni kwamba mabasi hayo yamewasili hivi karibuni bandarini hapo.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 20.3 kutoka Mbagala hadi Gerezani, ilijengwa na Kampuni ya Sinohydro kutoka China na ilikabidhiwa kwa Dart tangu Agosti 2023.
Katika awamu hiyo, kampuni ya kizalendo ya Mofat ndiyo imepewa mkataba wa miaka 12 kutoa huduma hiyo na mabasi yake yatatumia nishati ya gesi asilia.
Julai 22, 2025, Mtendaji Mkuu wa Dart, Dk Athuman Kihamia alisema mabasi hayo yangewasili kabla ya Agosti 15 na yatafuata mengine.
“Julai 20, nilishuhudia mabasi 99 yakipakiwa pale China tayari kuanza safari kuja nchini. Tunatarajia yatafika hapa ndani ya siku 20 hadi 21,” alisema Dk Kihamia, alipozungumza na Mwananchi mara baada ya kurejea kutoka China.
Endelea kufuatilia Mwananchi