WANANCHI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA WMA NANENANE

Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya NaneNane kitaifa mkoani Dodoma na kupatiwa elimu ya vipimo.

Pamoja na kupatiwa elimu ya vipimo, wananchi hao wanapata fursa ya kuuliza maswali ana kwa ana na kujibiwa na wataalamu pamoja na kuelekezwa kwa vitendo namna WMA inavyohakiki vipimo mbalimbali ili kumlinda mlaji.