WIZARA YA FEDHA YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA MISAMAHA YA KODI NANENANE

Afisa
kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha
(kushoto), akitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma, kuhusu ripoti
ya hali ya Uchumi ya nchi mwaka 2024 kwa wakazi wwa jiji la Dodoma, walipofika
kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika
Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi
Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025. 

Kamishna
Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi.
Dionisia Mjema (kulia), akikabidhiwa vipeperushi vya huduma zinazotolewa na
Kitengo cha Mkataba cha Wizara hiyo na Mkutubi Mwandamizi wa kitengo hicho, Bw.
Fredy Mpoma, wakati alipofika kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye
Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini
Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo
na Uvuvi 2025.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi Uhasibu Tanzania, Prof. William Pallangyo (kulia),
akifurahia jambo baada ya kuelezwa na Afisa Ugavi Mwandamizi wa Idara ya Sera
za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Anne Swila (kushoto), namna ambavyo
Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi unafanya kazi, wakati alipofika kutembelea Banda
la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya
Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025. Katikati ni Afisa Ugavi wa Idara ya
Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi.

Maafisa
Tehama Wandamizi Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga (kulia) na Bi. Zaina
Mwanga (Katikati), wakimkabidhi vipeperushi vya Mfumo wa Ulipaji wa Huduma za
Serikali (GePG), Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Paul Bundala, alipofika kutembelea
Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja
vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

Afisa
Biashara na Uendeshaji Kampuni ya Uwekezaji wa UTT, Bi. Pili Kunambi (Kushoto),
akitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma, kuhusu namna ya kufungua
akaunti ya UTT, kuangalia Taarifa fupi ya akaunti, na namna ya kununua vipande
kupitia UTT Sim Invest (Uwekezaji Kiganjani), wakati walipotembelea Banda la
Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya
Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

Afisa
Masoko wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Andew Punjila (kushoto), akitoa
elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Kikuyu, kuhusu umuhimu wa
takwimu katika kupanga na kufanya maamuzi katika shughuli za serikali, wakati
walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa
katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua
Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

 (Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

.………………………

Na
Josephine Majura na Joseph Mahumi, WF, Dodoma.

Wananchi
wamehimizwa kufika kwa wingi katika Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya
Kilimo (Nanenane) Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini
Dodoma, ili kupata elimu kuhusu misamaha ya kodi inayotolewa na Serikali katika
Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kama chachu ya kukuza sekta hizo nchini.

Wito
huo umetolewa na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Fedha, Wizara
ya Fedha, Bw. Fronto Furaha, alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea
Banda hilo. 
 

Alisema
kuwa ni muhimu kwa wananchi wanaojihusisha na kilimo, ufugaji na uvuvi kufahamu
haki na wajibu wao katika mfumo wa kodi, pamoja na kufahamu fursa ya misamaha
mbalimbali ya kodi iliyotolewa katika kilimo, ufugaji na uvuvi.
 

“Tunaalika
wananchi wote kutembelea Banda letu ili kupata uelewa mpana kuhusu aina
mbalimbali za misamaha ya kodi inayotolewa, masharti ya kuipata, pamoja na
taratibu sahihi za kunufaika na misamaha hiyo,” alisema Bw. Furaha.
 

Alibainisha
kuwa lengo kuu la utoaji wa elimu hiyo ni kuwajengea wananchi uelewa wa kina
juu ya nani anayestahili kupewa msamaha wa kodi, kwa nini misamaha hiyo
hutolewa, na athari chanya inazozalisha katika uchumi na maendeleo ya kijamii.
 

“Kuna
dhana potofu miongoni mwa baadhi ya wananchi kuwa misamaha ya kodi hutolewa kwa
upendeleo au watu maalum tu, tunataka kuondoa dhana hiyo kwa kutoa elimu ya
kina kuhusu vigezo vinavyotumika na namna ya kunufaika kupitia mifumo ya
Serikali,” alifafanua Bw. Furaha.

Aidha,
Bw. Furaha, alieleza kuwa misamaha hiyo inalenga kuhamasisha uwekezaji katika
sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ambapo pembejeo na viuatilifu vya kilimo,
vifaa vya uvuvi na mifugo vinavyoingizwa nchini kwa ajili ya sekta hizo,
vinapewa misamaha kulingana na taratibu na sheria, ambapo misamaha hiyo
imeendelea kuwa chachu kwa sekta hizo kuendelea kuongeza mchango wake katika
ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.
 

Aliainisha
kwa mifano, baadhi ya pembejeo za kilimo, mitambo ya uchakataji wa mazao ya
kilimo, viuatilifu vya kilimo, vifaa vinavyotumika katika uvuvi kama nyavu za
uvuvi na vifaa vinavyotumika katika ufugaji vinapewa msamaha wa kodi kwa
maendeleo ya sekta hizo, ambayo moja kwa moja yanagusa maisha ya wananchi wa
kawaida.
 

Baadhi
ya Wananchi waliotembelea Banda hilo walieleza kufurahishwa na elimu
waliyoipata, ambayo imewasaidia kuelewa zaidi kuhusu jinsi wanavyoweza
kunufaika kisheria na misamaha ya kodi, na pia kuchangia katika kukuza uchumi
wa Taifa kwa kufuata taratibu sahihi.

Wizara
ya Fedha imeahidi kuendelea kushirikiana na wananchi kwa kutoa elimu kupitia
maonesho, semina na mikutano ya hadhara, ili kuhakikisha wananchi wanakua na
uelewa mpana wa masuala ya misamaha ya kodi.

Wizara
ya Fedha pamoja na Taasisi zilizo chini yake inashiriki katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu
“Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025’’.