Rais Samia Kuchukua Fomu ya Urais Kesho – Global Publishers



Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amesema kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu atachukua fomu ya Urais kesho Agosti 9, 2025 katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi Dodoma akiambatana na Mgombea Mwenza Dkt. John Nchimbi.