VETA YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA KUNDI LA WANAWAKE NA SAMIA

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepongezwa kwa kuendelea kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia Mpango wa mafunzo unaotekelezwa na Taasisi ya Wanawake na Samia.
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 7 Julai, 2025 na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule ambae ndie muasisi wa Taasisi hiyo, alipotembelea banda hilo la VETA lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane), Nzuguni, jijini Dodoma na kuongea na wahitimu wa Mafunzo hayo wanaoonesha bidhaa mbalimbali walizotengeneza baada ya kupata mafunzo kutika vyuo vya VETA.
“Tunafahamu fika kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (Dkt. Samia Suluhu Hassan) amekuwa akihimiza utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa makundi maalum wakiwepo wanawake. Naipongeza VETA kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwa tunaona matokeo yake kupitia bidhaa na bunifu mbalimbali zinazofanywa na wanawake hapa Dodoma na kote nchini,” amesema Senyamule.
VETA imeendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa Taasisi ya Wanawake na Samia kupitia vyuo vyake kote nchini.