INEC YAKABIDHI FOMU ZA UTEUZI KWA MGOMBEA WA KITI CHA RAIS WA CHAMA CHA MAPINDUZI

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mgombea huyo wa CCM alichukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. 

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakionesha mkoba wa fomu za kuomba kuteuliwa na Tume kuwania Kiti cha Rais na Makamu wa Rais katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu baada ya kupokea fomu.

Mgombea Mwenza wa Chama cha Mapinduzi, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu baada ya kupokea fomu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akisoma barua kutoka Chama cha Mapinduzi inayowatambulisha wagombea wa chama hicho.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akifuatilia tukio la utoaji fomu za uteuzi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele  akitoa mwongozo wa nyaraka ambazo Tume inazikabidhi kwa mgombea. 

Sehemu ya Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika zoezi la utoaji fomu za uteuzi.