RAIS SAMIA AIPA KONGOLE TADB KWA UTENDAJI


 :::::

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa utendaji mzuri ulioleta tija kwa wakulima.

Ameyasema hayo leo Agosti 8, 2025 wakati akihutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya Nane Nane Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Rais Samia amesema utendaji mzuri wa Benki hiyo umeipa uwezo  wa kuwezesha wananchi na kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Maadhimsho ya Nane Nane Kitaifa yanafanyika Dodoma na yameshirikisha wakulima, wafugaji na wavuvi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.