TADB YAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUIWEZESHA KUKUZA MTAJI

::::::

Na mwandishi wetu,Dodoma

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika uwezeshaji wakulima kwa kuwapatia mikopo ya Pembejeo.

Akitoa maelezo kwa Mhe. Rais Samia kuhusu utendaji wa Benki hiyo leo Agosti 8,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Nane Nane kitaifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Frank Nyabundege amesema mtaji wa Benki hiyo umekuwa kutoka bilioni 60 hadi bilioni 442.

“Benki yetu itaendelea kudhamini maonesho ya NnNe Nane kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kwa sababu imeiwezesha kuwa na mtaji mkubwa,” alisisitiza Nyabundege.

Mgeni rasmi katika maonesho ya Nane Nane Kitaifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.