:::::::::
Morogoro, tarehe 08/08/2025
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imenyakua kombe kupitia maonesho ya Nane Nane 2025 yaliyofanyika katika Mkoa wa Morogoro. Ushindani wa TMA kupitia kundi la ushindani lililohusisha taasis za Serikali upande wa Mawakala na Mamlaka za Serikali nchini, umeifanya TMA kuibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili kwenye ambapo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ilishika nafasi ya kwanza na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikishika nafasi ya tatu.
Aidha, TMA imelipokea kombe hilo kwa furaha kubwa na kutoa shukrani zao za dhati kwa waratibu wa maonesho hayo kwa kutambua mchango mkubwa wa TMA katika kuhudumia wadau mbalimbali kwenye maonesho hayo, ambapo wageni zaidi ya 2942 wameweza kuhudumiwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ya sayansi ya hali ya hewa.