Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, tarehe 10 Agosti 2025.
Rais Samia aliwasili kuongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai, aliyefariki dunia hivi karibuni. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.