Serikali yatangaza nafasi za ajira

Dar es salaam. Serikali kupitia ofisi ya Rais sekretatieti ya ajira katika utumishi wa umma imetangaza nafasi 73 za ajira kwa raia wa tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa waliopo kazini serikalini. mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni Agosti 21, 2025.

Kwa mujibu wa tangazo la ofisi hiyo, la  Agosti 8, 2025 Katibu wa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma kwa niaba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo kama ilivyoainishwa katika tangazo hilo.

Nafasi hizo zinajumuisha, mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa hesabu), nafasi 55. sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza ya biashara/sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu au stashahada ya juu ya uhasibu pamoja na shahada ya kwanza/stashahada ya sayansi ya menejimenti ya kodi kutoka vyuo au taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

Nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii (ukaguzi ya usalama wa mifumo ya (Tehama) nafasi tano.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu katika mojawapo ya fani ya usalama wa mtandao (bachelor of cyber security), usalama wa mifumo ya Tehama  (bachelor of ict security) au usalama wa mtandao wa kompyuta (bachelor of computer network security) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali, pia wenye cheti cha Certified Ethical Hacker (CEH), Cisco Certified Network Associate in Security (CCNA).

Nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa kiuchunguzi fani ya utengenezaji wa programu za Tehama) nafasi moja.

Sifa za mwombaji awe na  shahada ya kwanza /stashahada ya juu ya Tehama katika fani ya utengenezaji wa programu za mifumo ya Tehama kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali na ufahamu na maarifa ya vitendo katika java ee, c#, c++ na python pamoja na uwezo wa kufanya kazi za mifumo ya uhifadhi data (Relational Database Management Systems (RDMS).

Mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi- fani ya usanifu wa majengo (architecture) nafasi moja.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza /stashahada ya juu ya usanifu wa majengo (bachelor of architecture) kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali na waliosajiliwa na bodi za usajili ya fani husika.

Nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi- fani ya uhandisi wa mitambo (mechanical engineer) nafasi moja.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza /stashahada ya juu ya uhandisi mitambo (bachelor of mechanical engineering) kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

Nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi- fani ya uchumi (economist) nafasi tatu.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu katika mojawapo ya fani zifuatazo: sayansi ya uchumi, sayansi ya takwimu na sayansi ya uchumi kilimo kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

Nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii (ukagiuzi wa ufanisi- mhandisi wa ujenzi) nafasi tatu.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza/stashahada ya juu ya sayansi katika fani ya uhandisi wa ujenzi (bachelor of science in civil engineering) kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

Pia nafasi nyingine ni mkaguzi daraja la ii, (ukaguzi wa ufanisi fani ya uhandisi wa migodi) nafasi moja.

Sifa za mwombaji kuajiriwa wenye shahada ya kwanza/stashahada katika fani ya sayansi ya uhandisi wa madini kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Pia, mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi – fani ya mipango miji (town planner) nafasi moja.

Sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu katika fani ya sayansi ya upangaji miji na maeneo ya ardhi (urban and regional planning) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

Mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi-fani ya uhandisi wa umeme) nafasi moja. sifa za mwombaji awe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu katika fani ya sayansi ya uhandisi wa umeme (bachelor of science in electrical engineering) kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

Mkaguzi daraja la ii (ukaguzi wa ufanisi-fani ya uhandisi wa mawasiliano) nafasi moja sifa za mwombaji kuajiriwa wenye shahada ya kwanza au stashahada ya juu katika fani mojawapo ya sayansi ya uhandisi wa mawasiliano (telecommunication engineering) kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

Tangazo hilo lilitaja masharti ya jumla yakieleza waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.

Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao, kwa ajili ya taarifa kwa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma.

Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria/wakili. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.

Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (detailed c.v) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na mwanasheria/wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha nne, kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

Hati za matokeo za kidato cha nne na sita havitakubaliwa.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama (TCU, NECTA na NACTE). Waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha katibu mkuu kiongozi.

Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka na cac. 45/257/01/d/140 wa Novemba 30, 2010.

Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. Vilevile mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni Agosti 21, 2025.

Tangazo hilo limesisitiza kuambatanisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, S. L. P. 2320, Dodoma.

Pia, maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (recruitment portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘recruitment portal’) (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘recruitment portal’.

Aidha, maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayatafikiriwa.