MCL, Vodacom waandaa majadiliano kuchochea athari chanya Tanzania

Dar es Salaam. Alhamisi ya  Agosti 14, 2025 kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT), Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania itakuwa mwenyeji wa majadiliano muhimu ya mtandaoni kujadili ‘Kuchochea Athari: Ushirikiano kwa Ajili ya Watu, Sayari na Ustawi’.

Majadiliano hayo ya mtandaoni yatawakutanisha viongozi wenye maono, wataalamu, na wakereketwa wa mabadiliko kujadili jinsi mawasiliano na mipango yenye malengo mahususi inavyokuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi yenye maana kwa Tanzania.

Vodacom Tanzania imekuwa nguzo ya mawasiliano kwa zaidi ya watu milioni 25 nchini, ikitumia teknolojia kuwezesha jamii na kuondoa pengo la upatikanaji wa huduma. “Dhamira yetu inakwenda mbali zaidi ya upatikanaji wa mtandao,” anasema Zuweina Farah, Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania Plc.

“Tunatumia teknolojia kufungua fursa katika elimu, afya, kilimo na zaidi, huku tukisonga mbele kufanikisha Dira ya Tanzania 2050 ya maendeleo endelevu na jumuishi.”

Mwananchi Communications Limited, ahadi yetu ya Kuliwezesha Taifa kwa kujitolea kwetu kusimulia habari muhimu na athari chanya, ubunifu, na zenye matumaini. “Kwa kupaza sauti na hadithi hizi, tunachochea mazungumzo yanayohamasisha hatua za pamoja na ukuaji endelevu,” anasema Edson Sosten, Mkuu wa Masoko, Masuala ya Kampuni na Uendelevu.

Washiriki watapata maarifa kuhusu jinsi ushirikiano wa mawazo kati ya sekta za umma na binafsi, jamii na viongozi unavyoweza kuchochea athari endelevu, kusaidia Tanzania kujenga mustakabali imara na wenye ustawi kwa wote.

Tunakuomba uwe sehemu ya mazungumzo haya muhimu na kuungana nasi kuendesha mabadiliko chanya.

📅Tarehe: Alhamisi, 14 Agosti 2025
🕒Muda: Saa 8:00 mchana – Saa 9:30 alasiri EAT
🔗Jisajili hapa:https://bit.ly/4lqzeO7