Piku yazinduliwa rasmi, mmoja akijishindia vitu lukuki

Dar es Saalam. Kadri serikali inavyochukua hatua kuhakikisha kuwa utafiti na ubunifu vinakuwa chachu kuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, baadhi ya wavumbuzi wa Kitanzania wameunga mkono maono hayo kwa kuzindua jukwaa jipya la kidijitali linaloitwa Piku.

Jukwaa hilo la Piku ambalo lilizinduliwa rasmi Agosti 7, 2025 jijini Dar es Salaam linafanya kazi kwa mfumo wa mnada unaotoa fursa kwa watanzania kucheza kwa kuweka dau la chini la kipekee na hatimaye kujishindia vifaa mbalimbali vya thamani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Uendeshaji wa Biashara wa Piku, Sia Malewas, alieleza kuwa Piku imepatiwa leseni maalum na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

“Wavumbuzi walioanzisha jukwaa hili walitaka kuunda kitu tofauti kitu kinachochochea fikra, kinachovutia na kinachowapa Watanzania njia ya kipekee ya kujishindia zawadi,” aliongeza Malewas.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari na Mawasiliano, Barnabas Mbunda amesema Piku ni jukwaa la kidijitali linalohusisha vijana na watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea ambapo mshiriki anaweza kupakua App ya jukwaa hilo kwenye simu za adroid kwa kuingia kwenye ‘play store’.

Amesema washiriki wanaweza kununua tiketi kwa bei nafuu kuanzia Sh.1,000 kwa tiketi 10, sh 5,000 kwa tiketi 50, sh. 10,000 kwa tiketi 100, na kuendelea hadi Sh100,000, ambapo nafasi ya ushindi huwa kubwa zaidi.

“Tofauti na majukwaa mengine au minada ya kawaida inayojulikana, Piku unafanya kazi kwa njia ya kipekee kabisa kwani mshindi ni yule aliyeweka dau dogo na la kipekee ambalo halijarudiwa na mshiriki mwingine yeyote. Hii inamaanisha kwamba kila mshiriki ana nafasi ya kipekee ya kushinda bidhaa za thamani kwa gharama ndogo kabisa,” amesema Mbunda

Katika siku ya kwanza ya uzinduzi Mjasiriamali Sabri Hamis mwenye makazi yake Zanzibar alijishindia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh5 milioni baada ya kuibuka mshindi katika jukwaa jipya la kibunifu lijulikanalo ‘Piku’.

Hamis kupitia jukwaa hilo alijishindia Televisheni ya inchi 55, Kiyoyozi na kifaa cha muziki vyote kutoka LG, king’amuzi cha DSTV kilicholipiwa mwaka mzima pamoja na kifaa cha internet (router) kilicholipiwa mwaka mzima kutoka Airtel.

Hamis ambaye ndio mshindi wa kwanza katika jukwaa hilo tangu kuzinduliwa kwake amesema amefurahishwa na ujio wa jukwaa hilo lenye lengo la kuwainua vijana na wajasirimali mbalimbali.

“Mimi nimecheza mara moja na nimetumia sh.1000 tu ambayo imeniwezesha kushinda vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni tano, hakika hii ni nguvu ya buku na kweli nimeamini elfu moja ina nafasi ya kubadili maisha yako. Niwaombe watu wapakue hiyo app na kucheza kwani maisha yanaweza kugeuka kwa dau moja tu,” amesema Hassan

Kwa upande wake Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Lucy Katamba amesema jukwaa hilo limechezeshwa vizuri na mshindi amepatikana kwa haki huku akisisitiza kuwa sekta ya michezo inakua na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.