Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UDP, Saumu Rashid, akiwa na Mgombea mwenzi wa , Salim, Juma Khamis Faki,wakiwa wamenyanyua mikono juu kuashiria ushindi walioupata kwa kuchaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha UDP.
.jpeg)
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UDP, Saumu Rashid akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya Chama hicho.
Dar es Salaam, Agosti 11, 2025
CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi wagombea wake kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mgombea Mwenza, pamoja na Urais wa Zanzibar, katika Mkutano Maalum wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wagombea waliotangazwa ni: Saumu Rashid, Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Juma Khamis Faki, Mgombea Mwenza Naima Salim Hamad – Mgombea wa Urais wa Zanzibar
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 390 kutoka mikoa 30 ya Tanzania Bara na Visiwani. Saumu Rashid alipata ushindi mkubwa kwa kupata kura 376 za ndiyo dhidi ya kura 14 za hapana, akichaguliwa rasmi kupeperusha bendera ya UDP katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, aliwataka wagombea wake kushirikiana kwa karibu katika kampeni, huku wakihubiri upendo na mshikamano badala ya chuki, kwa lengo la kulinda amani ya nchi.
“Nchi hii ni yetu, hatuna mahali pa kukimbilia. Tanzania ndiyo kwetu. Tuiweke salama na tuendelee kuienzi amani yake. Chama ni watu; bila watu hakuna chama,” alisema Cheyo.
Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sist Nyahonza, aliwapongeza wajumbe wa UDP kwa kuendeleza demokrasia kwa amani. Alisisitiza kuwa demokrasia ni kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa, na kuitaka jamii kuendeleza moyo wa utulivu kipindi chote cha uchaguzi.
UDP inakwenda kwenye uchaguzi mkuu kwa kauli mbiu yake:
“Imarisha Demokrasia, Tunza Amani.”