Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele, leo Agosti 12, 2025, amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma.
Mhe. Mwalimu aliwasili kwenye ofisi hizo akiwa ameambatana na mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya chama hicho, Mhe. Devotha Mathew Minja.